Abdulhalim M. Mzale

Director Message


Bohari kuu ya Dawa Zanzibar ni moja kati ya taasisi za Wizara ya Afya yenye jukumu la kupokea, kuhifadhi na kusambaza Dawa muhimu, Vifaa tiba, Vifaa vya uchunguzi wa Kimaabara na uchunguzi wamionzi. Mara baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilitangaza Sera ya kutoa huduma za afya kwa wananchi wote bila ya malipo. Miongoni mwa maeneo muhimu ya huduma hizo ilikuwa ni pamoja na upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na bidhaa za afya. Usimamizi wa huduma hizi uliwekwa chini ya Idara tofauti zikiwemo Idara ya Mipango na Uendeshaji, Idara ya Tiba na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu katika Wizara iliyohusiana na Afya. katika kuongeza ufanisi wa huduma za dawa nchini, mwaka 2011 Bohari ilipandishwa hadhi kuwa Idara kamili na kupewa jukumu la kupokea, kusimamia, kuhifadhi na kusambaza dawa, vifaa tiba na bidhaa za afya.